Ministry of Water

Chato Water Supply and Sanitation Authority

(CHAWASSA)

ENEO LA HUDUMA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Chato ni Mamlaka iliyoanzishwa mnamo Mwaka 2018 na inafanya kazi kwa mujibu wa Sheria ya Maji na Usafi wa MazingiraNa.5 ya mwaka 2019. Eneo la huduma za Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Chato linajumuisha kata Tatu ambazo ni BWINA, CHATO KATI pamoja na MUUNGANO.

DIRA NA DHAMIRA

DIRA
Dira ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira CHATO (CHAWASSA) ni kuwa na Mamlaka ya Maji yenye uwezo wa kutoa huduma bora ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira nchini Tanzania.
DHAMIRA
Kutoa maji yakutosha, yanayokubalika kwa bei nafuu kwa huduma ya maji na usafi Mazingira kwa wakazi wa Chato Mjini..

MAADILI YA MSINGI

  • Kufanya kazi kwa ushirikiano.
  • Kufanya kazi kwa ufanisi na kujituma.
  • Kufanya kazi kwa kuzingatia muda na mpango kazi.
  • Kuzingatia maadili ya kitaalam.
  • Kutoa huduma kwa uwazi.
  • Kutoa huduma kwa uadilifu na uaminifu.
  • Kufanya kazi kwa Pamoja.
  • Kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.
  • Kuzingatia matumizi bora ya rasilimali za serikali.
  • Kujiheshimu na kuheshimiana.

HUDUMA ZITOLEWAZO CHAWASSA

Zifuatazo ni Huduma zitolewazo na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Chato
  • Kusambaza maji katika mitaa ya Mji wa Chato na vitongoji Vyake kwa kulaza mtandao wa mabomba ambayo mteja anaweza kuunganishiwa
  • Kusajili wateja wapya wanaohitaji huduma ya maji katika Mji wa CHATO
  • Kupokea Na kujibu hoja /malalamiko mbalimbali ya wateja na wadau wengine kwa ujumla
  • Kufanya matengenezo ya mtandao wa mabomba yanayoharibika au yanapoharibiwa ili huduma ya maji iendelee kutolewa kwa wateja kwa muda muafaka.
  • Kudhibiti wizi wa maji kwa kufuatilia kwa karibu matumizi ya maji kwa wateja wetu kwa kufanya ukaguzi wa kushtukiza.
  • Kufanya mawasiliano mbalimbali na wadau
  • Kuratibu utunzaji wa Rasilimali na miundo mbinu ya maji katika Mji wa CHATO.
  • Kukusanya maduhuli kutoka kwa wateja
  • Kuandaa na kusambaza ankara (Bills) za maji kila mwezi kwa wateja wetu.
  • Kusitisha huduma kwa wateja wote wasiolipia ankara zao kwa kipindi kinachozidi siku saba (7) tangu tarehe ya mwanzo ya kupokea ankara.
  • Kusoma dira za wateja kila tarehe 15 mpaka 18 ya kila mwezi husika.

WAJIBU WA MAMLAKA KWA WATEJA.

  1. Kutoa huduma bila upendeleo.
  2. Kutoa huduma kwa mujibu wa viwango vya ubora.
  3. Kutoa taarifa sahihi na kwa lugha inayoeleweka kirahisi.
  4. Kushirikisha wateja na wadau mbalimbali katika kuboresha utoaji wa huduma ya maji.
  5. Kujenga mahusiano mazuri na wateja.
  6. Kupokea, kusikiliza na kushughulikia masuala yote yanayoletwa na wateja.
  7. Kutoa elimu kwa wateja kuhusu huduma zitolewazo na mamlaka ya maji.
  8. Kuwashirikisha wateja wakati wa usomaji wa dira za maji na uandaaji wa ankara za maji.
  9. Kuhakikisha kuwa huduma ya maji inakuwa endelevu ikiwa ni pamoja na kutunza vyanzo vya maji, kuweka na kutekeleza mipango ya kuendeleza vyanzo vya maji na kutunza mazingira.
  10. Kuzingatia kanuni zote za uendeshaji wa mamlaka za maji ikiwa ni pamoja na kutowakatia wateja huduma ya maji siku za sikukuu, Ijumaa baada ya saa sita mchana, Jumamosi na Jumapili.

WAJIBU WA WATEJA KWA MAMLAKA

  1. Kulipa ankara kwa wakati ili kuifanya Mamlaka iwe na uwezo wa kuboresha huduma kwa wateja wake.
  2. Kutoa ushirikiano kwa watumishi wa Mamlaka wanaowahudumia.
  3. Kutoa maoni kuhusu mipango na huduma zitolewazo na Mamlaka.
  4. Kuhudhuria mikutano inayoitishwa na Mamlaka ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi.
  5. Kutoharibu miundombinu ya majisafi na usafi wa mazingira.
  6. Kutoa taarifa kuhusu uharibifu wa miundombinu na vyanzo vya maji.
  7. Kutoa taarifa kuhusu uvujaji wa majisafi na majitaka.

AINA ZA WATEJA WA MAMLAKA

Wateja wetu wamegawanyika katika makundi manne
  1. Watumiaji wa majumbani
  2. Wafanyabiashara
  3. Taasisi Mbalimbali za Kiserikali na zisizo za kiserikali
  4. Viwanda

MAADILI YA MSINGI

  1. Kufanya kazi kwa ushirikiano.
  2. Kufanya kazi kwa ufanisi na kujituma.
  3. Kufanya kazi kwa kuzingatia muda na mpango kazi.
  4. Kuzingatia maadili ya kitaalam.
  5. Kutoa huduma kwa uwazi.
  6. Kutoa huduma kwa uadilifu na uaminifu.
  7. Kufanya kazi kwa Pamoja.
  8. Kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.
  9. Kuzingatia matumizi bora ya rasilimali za serikali.
  10. Kujiheshimu na kuheshimiana.

NJIA ZA KULIPA ANKARA YA MAJI

  • Wateja watatumiwa Ankara kila mwezi Na wanaweza kufanya malipo kupitia Bank, simu za kiganjani, yaani Kwa njia ya (Vodacom, Tigo pamoja Na Airtel) au kufika kwenye ofisi za Mamlaka

MAONI NA MALALAMIKO YA WATEJA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Chato inapokea na kushughulikia malalamiko kuhusu utoaji wa huduma. Mteja anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa kutumia njia zifuatazo:
  1. Kufika Ofisi za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira zilizopo Mkuyuni
  2. Kuandika barua pepe (barua@chawassa.go.tz)
  3. Kuandika katika daftari la Malalamiko lilipo katika ofisi za Chawassa.

HAKI ZA MAMLAKA

Ili kuboresha huduma zetu wateja wetu wana haki na wajibu kama ifuatavyo;
  1. Kulipwa kwa wakati ankara za huduma ya maji na uondoaji wa majitaka
  2. Kusitisha huduma ya maji kwa mteja asiyelipa kwa wakati (siku 30 baada ya kumpatia notisi/ankara).
  3. Kupata taarifa sahihi na kwa wakati
  4. Mteja anaweza kusoma dira yake mwenyewe iwapo atapenda kufanya hivyo.
  5. Kupata huduma bora bila ubaguzi
  6. Kutoa / Kuwasilisha maoni, pongezi au malalamiko
  7. Kupata huduma bora na kwa wakati muafaka

HAKI ZA WATEJA

  1. Kupata huduma ya majisafi na uondoaji wa majitaka.
  2. Kupata taarifa sahihi na kwa wakati.
  3. Kutoa au kuwasilisha maoni, pongezi au malalamiko.
  4. Kupewa faragha na kutunziwa siri kuhusu huduma iliyotolewa.
  5. Kupata huduma bila kubaguliwa.
  6. Endapo mteja hatoshughulikiwa malalamiko yake kwa muda muafaka uliopo kwenye mkataba huu, au hataridhika anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa MKURUNGENZI MKUU – EWURA, S.L.P 285, DODOMA, au info@ewura.go.tz

MAWASILIANO

Kwa mawasiliano yote na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Chato tuma Kupitia anuani ifuatazo: -
  1. Anuani: S.L.P 98 BARABARA YA MKUYNI CHATO
  2. Simu: +25528292523
  3. E-mail:mchato@maji.go.tz au barua@chawassa.go.tz

UFUATILIAJI

  1. Taarifa juu ya ufatiliaji wa huduma zitatolewa kila baada ya malalamiko kuwa yametatuliwa kwa kuwasiliana moja kwa moja na mteja.

KUTOA TAARIFA KWA WATEJA

  1. Mrejesho wa utoaji wa huduma kwa wateja utapatikana kupitia matangazo mbalimbali au vipeperushi au kwa kuwasiliana moja kwa moja na Wataalam wa Mamlaka kupitia Na. +255(0)282982523 au Mkurugenzi Mtendaji kwa namba 0714977661 / 0620570556 au kwa watendaji wetu wa Huduma kwa wateja kuwapigia wateja moja kwa moja.

SAA ZA KAZI

  1. Tunapokea malipo ya Ankara za Maji masaa 24 kila siku kwa kupitia mfumo wa malipo ya serikali (Control number) unaowezesha malipo kufanyika muda wowote kwa njia ya mitandao ya simu, benki na mawakala.
  2. Tunapokea malalamiko kutoka kwa wadau wetu kila siku za kazi kuanzia saa 02:00 asubuhi – 10:00 Alasiri, Jumatatu – Ijumaa na saa 02:00 Asubuhi – 06:30 Mchana siku za Jumamosi (kwa njia za ana kwa ana, barua na kwa simu).
  3. Tunapokea maombi ya wateja wapya kila siku saa za kazi na kuzitekeleza ndani ya siku 7 baada ya mteja kulipia gharama zinazostahili. .
  4. Tunashughulikia hoja na malalamiko ya mteja kwa haraka iwezekanavyo tangu kupokea malalamiko kutoka kwa mteja wetu. .
  5. Tunashughulikia hoja na Malalamiko ya watumishi wa Mamlaka ndani ya siku moja.